BABA mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amefunguka juu ya mrembo anayetaka aolewe na mwanaye huyo.
Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar, Septemba 27, mwaka huu, Mzee Abdul, mkazi wa Magomeni Kagera, Dar alisema awali alimtaka Diamond aoe msichana asiye maarufu na alimtambulisha kwake, lakini msanii huyo akachomoa.Akasema baada ya Diamond kuchomoa, mwaka jana alimpeleka Wema nyumbani kwake na kumwambia ndiye chaguo lake.
“Niliwahi kumwonesha Diamond msichana wa kumuoa, lakini akampotezea, mwaka jana akaja na Wema akidai ndiye chaguo lake.
“Hata hivyo, baadaye nikasoma kwenye magazeti ameachana na Wema, sasa yupo na Jokate, mara nikasikia amerudiana na Wema, mara amepata mwingine Kenya, lakini mimi nasema, Diamond muoe Wema, ndiye mwanamke anayekufaa mwanangu,” alisema mzee huyo.
Akasema kigezo anachotumia kumkubali Wema ni kimoja tu, nacho ni hiki, msikie:
“Hata kama ana machafu yake, lakini Wema ni mwanamke muwazi, hafichi mapenzi, wengine wanaficha, wanakuwa na Diamond, lakini wakiulizwa na waandishi wanajibu ni uzushi. Sasa huu usiri kusema kweli si mzuri, kuna kitu kinafichwa katikati.”
Mwezi Agosti mwaka huu, mama mzazi wa Diamond naye alitoa tamko lenye mtazamo wake wa mrembo anayestahili kuolewa na mwanaye.
Mama huyo, Sanura Kasim ‘Sandra’, mkazi wa Sinza Mori, jijini Dar alisema si Wema (Sepetu) wala Jokate (Mwegelo) anayestahili kuolewa na mwanaye.
No comments:
Post a Comment