Twanga Pepeta imetoa mualiko Rasmi kwa wanamuziki wote waliopita chini ya mikono ya mama Asha Baraka "THE IRON LADY" Kuja kwenye TWANGA FACEBOOK FANS PARTY. Mialiko hiyo kwa wanamuziki wote Kuanzia MK SOUND ikiwa na kina Nyoshi El Sadat, Ellystone Angay, King Dodoo La Buchee, Rojer Muzungu, Lui Ka Toise na Bakunde, AFRICAN STARS BAND wakati ikipiga muziki kwenye Hoteli za kitalii wakati huo ikiwa na wanamuziki kama marehemu Asia Daruwesh na Andy Swebe pamoja na kina Amigolas, Mafumu Bilali, Patric Kamalee ambapo baadae ilibadilika na kuwa AFRICAN REVULUTION wana "chumvi chumvi Tutalamba" kubaki kuendelea kupiga muziki wa Hotelini za kitalii na AFRICAN STARS BAND kuja kupiga muziki wa uraiani na kubatizwa jina la TWANGA PEPETA ikiwa na waanzilishi kama vile Luiser Mbutu, Banza Stone, Rogert Hegga, Nyamwela, Danger boy, Aisha Mdinda, otilia, Mwantumu, Fatuma kiboroloni na Ally Choky (Extra Bongo), Deo Mwanambilimbi (Kalunde Band), Yahaya Mkango, Joseph Watuguru,Jesica Charles, Adolf Mbinga na Bob Gadi wako huru. MCD, Fergason, Lilian Internet,Chalz Baba na Ally Akida (Mashujaa Musica).
Pia tumetoa mialiko kwa wanamuziki waliopitia bendi nyingine zilizokuwa chini ya Asha Baraka ambazo ni pamoja na TAM TAM chini ya Mwinjuma Mumin, Badi Bakule, Seseme, Rashidi Mwenzingo, Amina Ngaluma "Japanesse" Queen Suzy, Aliyah (Fm Academia), Sweet baby (Mashujaa) Bob Kisa (Extra bongo), Endrew Sekidia (Akudo) na TWANGA CHIPOLOPOLO kina Hosea Bass, Hadija Kimobitel (Extra bongo) na wale wote waliokuwa VIBRATION SOUND kina Pasia Budas, Baba Isaya, Amos Mkono wa nabii, sele Kadance, Raja Ibrahim (Mashujaa Musica), Dispach (Fm Academia) na wengine wengi na jua itakuwa vigumu kuwakumbuka wote. KWAKUWA IDADI YA WANAMUZIKI WALIOPITA KWENYE MIKONO YA ASHA BARAKA NA TWANGA PEPETA NI WENGI .. INAWEZEKANA KUNA WENGINE WALIOSAHAULIKA WASIJISIKIE VIBAYA NAO WANAKARIBISHWA PIA.
No comments:
Post a Comment