LIBERATUS BARLOW ENZI ZA UHAI WAKE.
KAMANDA WA POLICE MKOA WA MWANZA BWANA LIBERATUS BARLOW AMEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAO HISIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO. MAREHEMU ALIUWAWA NJIANI MAJIRA YA SAA TISA USIKU AKIELEKEA NYUMBANI KWAKE AKITOKEA KWENYE KIKAO CHA HARUSI.
KUUWAWA KWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ,IGP MWEMA ATUMA KIKOSI MWANZA.
Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha kuuwawa kwa kakamnda wa Mwanza Liberatus Barlow .Amesema kuwa kamanda huyo wa polisi ameuwawa na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30 na saa 8 usiku katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.Mwema amesema kuwa kamanda Barlow alikuwa akitokea katika kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla alikutwa na tukio hilo la kupigwa risasi.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linataraji kuanza uchunguzi wake kuanzia leo na timu ya askari kutoka makao makuu ya polisi wataondoka mapema leo kwenda jijini Mwanza kuungana na askari wa mkoa huo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na msako wa majambazi hayo .Mwema amewataka wananchi wa Mwanza kutoa ushirikiano wao kwa jeshi la polisi ili kufanikisha zoezi hilo na kuwataka kutokuwa na hofu yoyote kutokana na tukio hilo.

No comments:
Post a Comment