INAWEZEKANA kwamba Tamasha la Fiesta 2012, lilikumbwa na matukio mengi ya aibu lakini lile la mwanamuziki Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’, kuvua nguo na kumwaga ‘lazi’ mbele ya maelfu ya Watanzania, likawa la funga kazi kuliko yote.
Diamond ambaye alishangiliwa vilivyo, wakati akitumbuiza na kudhihirisha kwamba yeye bado moto wa kuotea mbali anapokabidhiwa jukwaa, alipozidiwa na mzuka, alisaula suruali yake na kubakiwa na kivazi cha ndani ambacho wengi hukiita ‘boxer’ (chupi).
Mwanamuziki huyo, hakufanya hivyo peke yake, kwani aliposaula na wacheza shoo wake walimfanya vivyo hivyo, nao wakabakiwa na vi-boxer vyao.Chanzo cha habari ni sangafesto.blogspot.com
Hii ndio Ibilisi anavyofanya kazi yake. Lakini sijui hawa watu hawana Director, au meneja, wakuwaongoza, maana haya maswala ni muhimu kukawa na washauri, .....
ReplyDelete