MAJAJI wa shindano la Epiq BSS wiki hii wanatarajiwa kuwa walimu wa washiriki tofauti na wiki zilizopita, ambapo kulikuwa na walimu maalumu wa kuwafundisha washiriki hao pamoja na wasanii mbalimbali kutoka nje ya nyumba.
Hali hiyo, inatarajiwa kuleta ushindani mkubwa kati yao, hasa ukizingatia wao ndio wamekuwa na kazi ya kuwakosoa washiriki kila wanapopanda jukwaani.
Majaji hao, Salama, Madam Rita, pamoja na Master J wamegawiwa washiriki wa kuwafundisha, ambapo kila jaji amepewa washiriki watatu kati ya tisa waliobaki.
Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliahidi kuwa washiriki wake ndio watatisha wiki hii, kwani atawatoa nje ya kambi kabisa ili wakapate mafunzo maalumu.‘Hii ni mara ya kwanza majaji tunapewa kazi ya kuwafundisha vijana, hivyo tunatarajia watu wataona kama washiriki wetu watakuwa kama sisi tunavyotaka wawe,” alisema Ritha.
Naye Salama, alitamba kuwa atawafundisha washiriki wake ili wawafunike washiriki wote wiki ijayo.“Ntawapeleka washiriki wangu sehemu yoyote watakayotaka wajifunze, ili wiki ijayo wafunike washiriki wote,” alisema Salama.
Kwa upande wake, Master J, yeye alikuwa kimya, akionekana kutafakari kazi iliyo mbele yake.
Washiriki walioko kwenye kundi la Jaji Salama ni Meninah, Husna na Nshoma huku kwa Madame Ritha ni Walter, Wababa pamoja na Nsami naye Master J akiwa na Godfrey, Salma na Norman Severino.
No comments:
Post a Comment