Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume au wanawake kuwatelekeza watoto waliozaliwa nje ya ndoa na hivyo kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani , Ni vyema katiba ijayo ikaweka wazi jambo hilo ili kuwadhibiti wanaume wasizae ovyo na pia kuondoa watoto wa mitaani hayo yamesemwa na mkazi wa Rau Balbina alipokuwa akitoa maoni yake mbele ya Tume ya mabadiliko ya katiba mpya.
Habari na Adeladallykavisheblog. Hivyo ili kudhibiti watoto wanaozaliwa nje ya ndoa vipimo vya DNA vitumike kubaini baba halali na wawajibishwe kuwatunza kwani watoto wengi wa mitaani wametokana na wazazi kutengana au kukataliwa na wazazi wao hususani wanaume hivyo Katiba ikiwa na mwongozo kuhusu jambo hilo ni wazi kwamba tatizo la watoto hao litakwisha. |
No comments:
Post a Comment