Taarifa ziliripotiwa mapema leo kuwa lilikuwepo jaribio la kutaka
kuchoma moto jengo la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Usharika wa Yombo Vituka, Temeke Dar es Salaam, jaribio ambalo
halikufanikiwa ilivyokusudiwa.
Taarifa ya mmoja wa watu waliopepeleza ukweli wa taarifa hizo inasema,
“Nimeongea kwa simu na ndugu yangu anayeishi huko Yombo, kanisa lililochomwa ni KKKT ambalo huyo ndugu yangu anaabudu. Ila nasikia hawakufanikiwa kuchoma maana walipata upinzani toka kwa walinzi wawili wa kanisa, mmoja aligonga kengele kwa haraka watu wakaanza kukusanyika hivyo wale wahujumu wakakimbia. Ila nasikitika kwakuwa hawakukamatwa.”

No comments:
Post a Comment