EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, October 19, 2012

Miaka mitatu jela kwa kuiba mtoto.

Jackline Masinde, Geita
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa Wilaya ya Geita, imemtia hatiani Pendo Fikiri (20) mkazi wa Mtaa wa Mwembeni Kijiji cha Nyankumbu wilayani Geita baada ya kupatikana na hatia ya kuiba mtoto mwenye umri wa miaka sita kishirikina.

Katika hukumu hiyo, Pendo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na Hakimu wa mahakama hiyo, Zablon Kesase, baada ya kupatikana na hatia ya kumuiba mtoto huyo (jina linahifadhiwa) na kuishi naye nyumbani kwake katika kipindi cha wiki tatu huku akijua kuwa siyo wake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kesase alisema kuwa adhabu aliyoitoa kwa mshitakiwa imekusudiwa kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo hapa nchini na kuonywa watu wenye tabia kama hizo kuacha.

''Mahakama inamtia hatiani kwa kosa hili ambalo umekiri hapa wewe mwenyewe, hivyo hakuna shaka kwamba ulilitenda. Kosa ulilokiri ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 169 (1) (a) kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, hivyo pasipo kutilia shaka yoyote ninakuhukumu kwenda jela miaka mitatu ili liwe fundisho kwako,'' alieleza katika hukumu hiyo.
Awali akisomewa mashitaka na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Abner Wegoro, alidaiwa kwamba alitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu, majira na saa 6 mchana eneo la Mtaa wa Mwembeni wilayani humo.

Alisema, baada ya mshitakiwa kumuiba mtoto huyo kwa njia za ushirikina, aliishi naye kwa muda wa wiki tatu hadi wazazi wa mtoto huyo walipopata taarifa toka kwa majirani ambao walimsikia mtoto akilia toka nyumbani kwa huki wakitambua yeye hana mtoto.

Alisema kutokana na kupotea kwa mtoto huyo katika mazingira ya kutatanisha wazazi wake walilazimika kutoa taarifa kwa uongozi wa jeshi la sungu sungu kijijini hapo, ambapo Oktoba 17 mwaka huu, majira ya 5.00 asubuhi mshitakiwa huyo alikamatwa na kisha kufikishwa kituo cha polisi.

Akijitetea mahakamani hapo, mshitakiwa huyo aliwaacha hoi wasikilizaji baada ya kueleza kwamba alimuiba mtoto huyo kwa ajili ya kumtumia kishirikina lakini bahati mbaya alikamatwa na hivyo kuomba mahakama hiyo kumsamehe kwani alitenda hayo kutokana na mumewe kuwa mbali naye.

Licha ya utetezi wake huo, mahakama hiyo ilimtia hatiani na hivyo kutwaliwa na askari kupelekwa gerezani kwa ajili ya kuanza kutumikia kifungo chake.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate