EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 17, 2012

Ulimboka kutaja wabaya wake wote siku za karibuni.

Habari Na Mwandishi Wetu.
KIONGOZI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, amepanga kumwaga taarifa nyeti kuhusu kutekwa na kuteswa kwake na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, Bunju, jijini Dar es Salaam.Mmoja wa ndugu na rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka, ameliambia Mwananchi kuwa, kiongozi huyo wa jumuiya, amepanga kuanika hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari.Alisema Dk Ulimboka, atatumia mkutano huo kueleza siri ya kutekwa kwake.

“Siku yoyote kuanzia sasa umma, utafahamu ukweli halisi wa kilichompata kijana wetu. Niliongea naye juzi na amenithibitishia kuwa atakutana na waandishi wa habari na kueleza kila kitu katika  masahiba yaliompata,” alisema ndugu huyo wa Ulimboka ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake litajwe gazetini.
 lisisitiza  “Ni kweli kwamba Steven (Dk. Steven Ulimboka) amepanga kukutana na waandishi wa habari. Anataka kutumia mkutano huo, kuanika wote walioshiriki kumtesa, kumteka na kisha kumtupa katika msitu wa Mabwepande,”Alipoulizwa kuhusu kipya ambacho daktari huyo ataueleleza ulimwengu ambacho hakijafahamika, mwanafamilia huyo alisema: “Tuvute subira. Steven amepanga kutaja wote waliohusika katika kutaka kuangamiza maisha yake. Ameniambia kuwa anataka kuwaambia Watanzania ukweli wa kilichompata,”

Dk Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26 mwaka huu, katika maeneo ya Leaders Club jijini Dar es Salaam na baadaye kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikononi  na miguuni kabla ya kunyofolewa kucha na meno; katika Msitu wa Mabwepande.
Aliokotwa na wasamaria wema asubuhi yake na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Juni 30 kwa matibabu zaidi.

Tangu aliporejea nchini Agosti 12 mwaka huu, kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka ndani na nje ya nchi, kumtaka azungumze kwa madai kuwa kauli yake itasaidia kujulikana kwa ukweli kuhusu kilichompata.
Kufanyika kwa mkutano huo  kunatajwa na wachambuzi wa mambo kuwa kunaweza kuondoa kiwingu hicho, ikiwa ni pamoja na kujibu baadhi ya maswali yaliyobuka juu ya tukio hilo.
Katika mahojiano yake ya kwanza na gazeti hili, wiki iliyopita, Dk. Ulimboka alisema hali yake inaendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba anamshukuru Mungu na wote waliomuombea, ingawa bado anahitaji matibabu zaidi.“Madaktari wangu bado wanaendelea na uchunguzi kuhusu figo zangu ili waone kama zinaweza kufanya kazi au zinahitaji kuondolewa na kuwekwa nyingine. Lakini kwa jumla, hali yangu inaleta matumaini kidogo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate