MSANII nguli wa filamu Tanzania, Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Sister Mary’, iliyofanyika chini ya RJ Company ambayo itakuwa na nyota wengine kama Irene Uwoya,Johari na wengine kibao ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya filamu nchini.
Official cover ya filamu mpya ya ‘Sister Mary’
Ndani ya mzigo huoUwoya amecheza kama Sister Mary na Rayamecheza kama Father Criss.Ray alizungumza na kusema kuwa zipo filamu nyingine ambazo zinakuja lakini hiyo imeshakamilika na mashabiki wake wataanza kuitazama pia imetengezwa katika kiwango cha hali ya juu.
“Hiyo ndiyo filamu ambayo inakuja kwa sasa na nipo na wasanii wengi wazuri ambao wanafanya vizuri na kila msanii amecheza vizuri kulikana na nafasi yake, hata hivyo nawaomba mashabiki wangu wanipe sapoti yao kwani bila wao mimi siwezi kusimama na kufanya filamu,” alisema,
No comments:
Post a Comment