EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, October 11, 2012

Watumishi wanne wa Halmashauri wafukuzwa kazi.

Habari imeandikwa na Kennedy Kisula, HabariLeo, Lindi -- HALMASHAURI ya Wilaya ya Lindi mkoani Lindi imewafukuza kazi watumishi wake wanne akiwamo Mhasibu Mwandamizi kwa makosa mbalimbali mojawapo likiwa ni kusindikiza lori lililosheheni zao la korosho zisizolipiwa ushuru katika msimu wa mwaka jana.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Hijob Shenkalwah aliyasema hayo jana wakati alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kufunga mwaka wa fedha 2011/12, na kueleza kuwa watumishi hao walikuwa na makosa ya utoro kazini, kusindikiza lori la korosho na kutoa vizuizi njiani.


Alisema Mhasibu Mwandamizi wa halmashauri hiyo, Joseph Songoro anatuhumiwa kutenda makosa ya kusindikiza gari lililobeba korosho ambazo hazikulipiwa ushuru wa mamlaka hiyo. Alisema kosa hilo lilifanyika Novemba 27, mwaka jana na kuvunja kizuizi kilichopo Kijiji cha Madangwa kwa kutumia nguvu.Alisema kosa hilo kwa Sheria za Utumishi wa Umma, Kanuni ya 42, Songoro alikwenda kinyume cha Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003. Alifafanua zaidi, alisema Kanuni ya 42((1) jedwali la kwanza "A" inaeleza kuwa mtumishi akipatikana na hatia adhabu yake ni kufukuzwa kazi.

Mkurugenzi huyo alisema mtumishi mwingine ni Peter Kahisi ambaye ni Tabibu II katika Kituo cha Afya Rutamba alihusishwa na kosa la utoro kazini kuanzia Novemba 16 hadi Mei 17, mwaka huu.Alisema mhusika alipewa notisi na hati ya mashitaka ili ajieleze, lakini hakupatikana kwani hakuwapo katika kituo chake cha kazi na Kamati ya Uchunguzi ilithibitisha kutokuwapo kwake kazini.Alisema kwa kosa hilo alivunja kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 Kanuni ya 57 jedwali la kwanza "A" ambayo inaelekeza kuwa mtumishi wa umma akikosekana kazini kwa muda wa siku tano mfululizo bila ya sababu au kutotoa taarifa kwa mwajiri wake, atafukuzwa kazi.Alisema watumishi wengine ni Hamisi Lunda, Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Mnamba aliyekuwa mtoro kazini kuanzia Mei 28, mwaka jana hadi Mei 17, mwaka huu.Mwingine alikumbwa na kadhia hiyo ni Othmani Mrope ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Shuka utoro kazini kuanzia Oktoba 15, 2011 hadi kufikia Mei 17, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate