MDAU maarufu wa sanaa nchini, Allan Mmanyi ‘Captain Mupesa, amewataka
wasanii wa fani zote nchini kuwa na umoja na mshikamano ili kufikia
mafanikio yao.Mmanyi alitoa wito huo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ambapo
alisisitiza kuwa, endapo wasanii wataungana, wataweza kufikia mafanikio
kama ilivyo kwa wenzao wa nchi za Ulaya na Marekani.
Mdau huyo aliongeza kuwa, amekuwa akishangazwa na kuibuka kwa tabia ya wasanii kubaguana kutoka fani moja hadi nyingine.
Alilaani jambo hilo, kwani linaleta matabaka na kuitafuna sekta ya
sanaa hapa nchini na bila kuungana, kamwe hawataweza kufikia malengo ya
kukuza muziki na sanaa kwa ujumla hapa nchini.
“Wasanii wamekuwa na matabaka, kati ya wenye pesa na majina huku wale
ambao hawana fedha, wakijikuta wamejikunyata kama watoto yatima,
haipendezi kabisa,” alisema.
Aliongeza kuwa, hakuna ubishi wasanii hapa nchini, wamegawanyika kwa
mtindo usio na tija kwa tasnia yao, jambo linaloashiria kuanguka au
kukosa mwelekeo kwa biashara itokanayo na sanaa hapa nchini kama
hawatajirekebisha.
“Ni aibu sana... wasanii ni watu wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele
kuhamasisha jamii juu ya mambo mema, huku umoja likiwa ni jambo kuu,
lakini cha ajabu, siku hizi utakuta makundi ya mastaa wa filamu
yamejitenga kwa mafungu mafungu, wenye hela wako tofauti na wasio nazo,”
alisema Mmayi ambaye ni miongoni mwa wadau waliotoa ufadhili kwa
wasanii wengi hapa nchini.
Aliongeza kuwa hata wasanii wa muziki wa Bongo fleva, nao wanafanya
ujinga uleule wa kubaguana, kwani wapo wanaojiita wenye majina makubwa
na wale ambao bado hawajakamata ‘chati’ kutokana na uchanga wao au
kutopokewa vema na mashabiki
No comments:
Post a Comment