MRATIBU wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Sirila
Mwanisi, amewahimiza watu kujenga utamaduni wa kunawa mikono mara kwa
mara, ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Sirila alitoa wito huo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya
Siku ya Kunawa Mikono Duniani, sherehe ambazo zilifanyiwa katika
Viwanja vya Posta, Kijitonyama.Alisema watoto wadogo ndio wapo kwenye hatari zaidi ya kupata
magonjwa, hivyo ni lazima wazazi na walezi wakawaelimisha ili kuwaweka
katika mazingira mazuri.
“Watoto lazima waelimishwe namna ya kunawa mikono kabla na baada ya
kula, maana ndio nafasi ya kukabili vijidudu vya aina mbalimbali,
ukiwamo ugonjwa wa kipindipindu ambao ndio hatari zaidi,” alisema.
Katika maadhimisho hayo, wanafunzi zaidi ya 300 kutoka shule
mbalimbali jijini Dar es Salaam waliungana na wenzao duniani kuadhimisha
siku hiyo.Wanafunzi hao walifundishwa jinsi ya kukabiliana na uchafu wakati wote, sambamba na unawaji wa mikono kabla na baada ya kula.Maadhimisho hayo ambayo hufanyika Oktoba 15 ya kila mwaka, mwaka huu
yaliandaliwa na Kampuni ya PCB Witna na kudhaminiwa na sabuni ya Protex.
No comments:
Post a Comment