MKAZI wa Swaya, jijini Mbeya, Ndele Julius, anatafutwa na
polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na
ngumi.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, iliyotumwa
kwa waandishi wa habari jana, ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea
Novemba 25, mwaka huu, eneo la Swaya.
Taarifa hiyo ilimtaja mwanamke huyo aliyeuawa kuwa ni Sinjembele Julius (62), aliyekuwa mkulima.
“Chanzo cha kifo hicho ni mtuhumiwa kuwa na ugomvi na kijana mwenzake
ndipo mama yake alipokwenda kuamulia ugomvi na kugeukwa na mwanaye kisha
kuanza kushambuliwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.Ilielezwa kuwa baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikimbia, hivyo
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu au watu wenye taarifa juu ya mahali
alipo mtuhumiwa, ili akamatwe au ajisalimishe mwenyewe. Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya
No comments:
Post a Comment