EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, November 24, 2012

ASHA BARAKA AIFUNGUKIA ISHU YA MUUMINI MWINJUMA KUONDOKA TWANGA.

MKURUGENZI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ International juzikati ameifungukia ishu ya aliyekuwa muimbaji wa bendi yake, Muumini Mwinjuma kuwa alikuwa na haki ya kuondoka kwani hakuwa na mkataba wowote na Kampuni ya Aset.

Akizungumza na ‘kachala’ wa Funguka na Risasi ofisini kwake Kinondoni jijini Dar, Asha Baraka alisema tangu Muumini ajiunge na Bendi ya Twanga uongozi haukuwahi kuingia mkataba naye kwa sababu maalum ila alikuwa akipewa haki zake zote.

“Muumini alikuwa anafanya kazi na Twanga kama vile kusaidiana tu kutafuta chakula cha kila siku, angalau alikuwa akipata mshahara na posho lakini hatukuwahi kuingia naye mkataba kwani bado uongozi ulikuwa unafuatilia baadhi ya mambo.”
Funguka: Kwa hiyo unataka kuniambia Muumini alikuwa anapiga ‘deiwaka’ tu?
Asha Baraka: Siwezi nikasema hivyo wakati haki zake zote za msingi alikuwa anapata, tofauti ni kwamba hatukuwa na mkataba naye.
Funguka: Mbona kuondoka kwake kunafanana na uondokaji wa aliyekuwa mwanamuziki wako anayejulikana kwa jina la Venas au Anko Vena, hakuna kitu nyuma ya pazia?
Asha Baraka: Hapana hakuna kitu chochote, ninavyojua Muumini anaenda kujiunga na bendi moja hivi, nasikia inaitwa Victoria Band na Anko Vena nimeambiwa amejiunga na bendi iliyo chini ya Jeshi la Polisi, ndiyo maana nakwambia hakuna kitu kama hicho.
Endelea kufunguka  hii ndio nafasi ya kutoa dukuduku lako.
Asha Baraka: Kitu ambacho nampongeza Muumini ni pale aliponifuata na kuniambia ukweli kuwa anaondoka maana kuna sehemu amepata kazi. Nadhani kwake aliona kuna maslahi, hicho tu ndicho nampongeza kwani ameutendea haki ukongwe wake.
Funguka: Mbona unasema unampongeza kwa kuja kukuaga, kwani wanamuziki wote walioondoka hawajawahi kukuaga?
Asha Baraka: Chaz Baba aliniaga lakini kuna maneno alikuwa akiyazungumza sikuwa  napendezwa nayo. Vena hakuniaga, nilishtukia tu hayupo ila Muumini alitumia busara sana kwani alijua haya ni maisha, kuna kupanda na kushuka na ndio maana alikuja kuniaga.
Funguka: Ukiachana na ishu ya kuondoka kwa Muumini, mmejipanga vipi kuziba pengo la hao wanamuziki wawili walioondoka?
Asha Baraka: Bendi kama bendi iko vizuri sana, hivi ninavyoongea na wewe jioni wanamuziki wote wanaingia studio kurekodi nyimbo mbili, ya Kalala na ‘J 4’, ndio maana nakwambia bendi iko vizuri we’ mwenyewe shahidi.
Funguka: Kwa hiyo unataka kuniambia wapenzi wa Twanga Pepeta wategemee bonge la burudani Jumapili hii pale katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar?
Asha Baraka: Siyo burudani tu ila kutakuwa na ‘surprise’ ya nguvu kutoka kwa wanamuziki wa Twanga, ninachowaomba wapenzi wa Twanga wafike kwa wingi Dar Live maana burudani waliyokuwa wakiikosa zamani pale Viwanja vya Sigara TCC sasa imehamia Dar Live.
                                                   Chanzo ni Global Publishers.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate