LONDON, ENGLAND
RAFA Benitez, ambaye alikabidhiwa Chelsea Jumatano wiki hii huku akiwa na kazi ya kukutana na Manchester City kesho Jumapili, amesema atahakikisha anafanya mapinduzi makubwa ili kuwanyamazisha mashabiki wanaopinga uteuzi wake kuchukua nafasi ya Roberto Di Matteo.
Mashabiki wamekuwa wakisema kuwa hawamtaki kocha huyo wa zamani wa Liverpool kwa kuwa alikuwa hawapendi wakati alipokuwa Anfield na alikuwa akiapa kuwa kamwe hawezi kuinoa Chelsea.

Lakini Benitez amesema hajali kusikia tuhuma hizo na lengo lake ni
kuipaisha Chelsea. Pia kocha huyo hakuwa tayari kuomba radhi kutokana na
matamshi yake ya zamani.
Alisema: Kama ningekuwa shabiki ningemtaka kocha wangu apigane kwa ajili ya klabu.
"Mashabiki wanaweza kusema jambo lolote wanalotaka lakini wafahamu kuwa nipo kazini."
Lakini Benitez ana nafasi fupi ya kukisoma kikosi na kufanya mabadiliko madogo kabla ya kukwaana na Man City ambayo inataka kurudisha heshima baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya makundi.
Mhispania huyo ambaye aliiongoza Liverpool na kupata ubingwa wa Ulaya mwaka 2005 na kufika hatua ya fainali mara mbili kabla ya kutimuliwa mwaka 2010, amepewa kazi ya muda ya kuinoa Chelsea mpaka mwishoni mwa msimu, hiyo ni baada ya kocha Roberto Di Matteo kutimuliwa Jumatano wiki hii.
Di Matteo alifukuzwa baada ya Chelsea kuyumba katika mechi za karibuni huku kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Juventus kikiwa kipimo cha mwisho.
Benitez atatakiwa kusuka ngome nyingine baada ya mabeki wa awali kuruhusu mabao 21 kwenye mechi 10 za michuano yote.
Benitez ameungana na nyota wa Hispania, Fernando Torres, ambaye alisajiliwa katika klabu hiyo kwa ada ya pauni 50 milioni.
Awali Benitez na Torres walifurahia maisha wakiwa Liverpool baada ya kumsajili akitokea Atletico Madrid mwaka 2007.
Lakini Torres alishindwa kuonyesha kiwango kwenye kikosi ndio maana alikaa benchi kwenye mechi dhidi ya Juventus.
Baada ya kuanza kwa kasi, Chelsea imejikuta ikiangukia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na sasa inatakiwa kuamka kuanzia mechi ya kesho Jumapili.
Man City ina hasira baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia sare ya bao 1-1 na Real Madrid Jumatano wiki hii.
Kocha Roberto Mancini anaamini timu yake bado ni imara na inaweza kuinyoa Chelsea.
Nayo Manchester United, ambayo ipo nyuma ya Manchester City kwa pointi moja, iliwapumzisha wachezaji kadhaa kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray wiki hii sasa itashuka ikiwa kamili kucheza na QPR leo Jumamosi.
Wachezaji kama Rio Ferdinand, Wayne Rooney na Robin van Persie sasa wataingia uwanjani.
West Brom ambayo ipo nafasi ya nne iliwashangaza Chelsea baada ya kuwachapa mabao 2-1 wikiendi iliyopita na leo Jumamosi itakuwa na kibarua mbele ya Sunderland.
Kocha, Scot Clarke, ameonyesha mabadiliko baada ya kuwa kocha namba moja kwa mara ya kwanza kufuatia kuwa kocha wa pili katika vikosi vya Newcastle United, Chelsea, West Ham United na Liverpool.
Nayo Everton inayoshika nafasi ya tano, itaikaribisha Norwich City wakati Arsenal iliyo nafasi ya sita itacheza na Aston Villa.
Timu hiyo ina ari baada ya kutua kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:
Post a Comment