Kwa masikitiko makubwa
nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba
nimeiponda safu ya
uongozi na sekretariati ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti
lolote juu ya uongozi wa
CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi
huo. Ni vibaya kwa gazeti
lo lote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza
maoni yake. Kama ni
waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika.
Nasikitika sana kwa
waliokwazwa na hilo.
Askofu Kilaini.

No comments:
Post a Comment