PAROKO wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa Angelo Burgeo (60) na msaidizi
wake Herman Myalla (36) wamenusurika kufa baada ya kuvamiwa na majambazi
waliokuwa na silaha za moto, mapanga na nondo.
| Paroko |
| Paroko msaidizi |
Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako viongozi wamelazwa kwa ajili ya matobabu, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Faustine Gwanchele alisema Padri Myalla amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa kwa panga na nondo.
"Walifikishwa majira ya saa sita usiku wa kuamkia jana, na wakaanza kupatiwa matiababu wanayoendelea nayo mpaka sasa," alisema na kuongeza kwamba Padri Bergeo alianza kufanyiwa upasuaji jana ili kuondoa vipande vya risasi vilivyopo ndani ya mwili wake.
Tukio
hilo limetokea ikiwa siku moja tu baada ya mlinzi wa Kanisa Katoliki Kihesa
Iringa Mjini, Bathelomeo Nzigilwa (64) kujeruhiwa vibaya na majambazi
waliovunja kanisa hilo na kufanikiwa kuiba mali mbalimbali zikiwemo fedha
taslimu zaidi ya Sh 500,000.
Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.
Dk Gwanchelle alisema hali ya Nzigilwa ni mbaya kwasababu majambazi waliomjeruhi walimvunja mfupa wa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.
No comments:
Post a Comment