KOCHA wa muda wa Chelsea, Rafa Benitez amekaribishwa kwa sare ya bila bila dhidi ya Manchester City katika dimba la Stamford Bridge muda mfupi uliopita.
Benitez alilakiwa na mabango mengi yaliyomdhihaki wakati mchezo unaendelea, mengi kati ya mabango hayo yakisema “Benitez Out” huku mengine yakimsifia kocha aliyetimuliwa Roberto Di Mateo.
Hata hivyo Kocha huyo akizungumza kabla ya mechi hiyo, alimwagia sifa nyingi mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich.
Benitez alisema anaamini Roman Abramovich ni "mtu mzuri", baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza Alhamisi.
Benitez
alitumia "saa mbili au tatu" akiwa na mmiliki huyo wa Chelsea Alhamisi
jioni, baada ya kutangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu katika mkutano
na waandishi mapema siku hiyo.
Kocha huyo anaamini kuwa ataweza kufanya kazi vizuri na mmiliki huyo baada ya mazungumzo yenye tija.
Abramovich
ana sifa ya kutovumilia kushindwa - moja ya ushaidi wa hilo ikiwa
hatua yake ya hivi karibuni ya kumtupia virago Roberto Di Matteo -
lakini Benitez anaamini kwamba matakwa ya Abramovich hayana tofauti na
ya wamiliki na wenyeviti wake wengi wa zamani.
"Nina
miaka 26 katika uongozi wa klabu na naweza kuhakikisha kuwa nimekuwa na
wamiliki wengi tofauti na wenyeviti," Benitez alisema. "Kama una
ujasiri wewe binafsi na unaweza kujieleza mwenyewe, kila mtu anaweza
kuelewa.
"Maoni yangu kuhusu yeye (Abramovich), ni kwamba ni mtu mzuri. Unaweza kuzungumza nae. Anaelewa. "
Mhispania
huyo anasaema kuwa, anamuelewa vizuri Abramovich, kwamba ni mtu ambaye
anataka maamuzi ya kutenda zaidi kwa wafanyakazi wake badala ya kuweka
mbele dhana na hisia.
"Yeye
anapenda kuona ukiwa na wazo wazi: 'Nadhani ni wazi' kwa sababu ya hili
au lile, au hili haliwezekani kwa sababu ya hili au lile'," Benitez
aliongeza.
"Wakati
tukipata chakula cha jioni, ilivutia wakati tulipokuwa tukizungumza juu
ya kila kitu. Anajua mawazo yangu kuhusu (staili ya uchezaji ya) kukaba
nafasi, na yeye anajua kwa nini napendelea hili.
"Sote
tulizungumza. Kawaida mimi huzungumza sana. Kipaumbele cha mmiliki ni
kama mimi ni meneja mzuri, kocha mzuri, kama wachezaji wananielewa, kama
tutaweza kuwa timu ya kushinda. Yeye alikuwa wazi sana na hili."
Matokeo
ya mechi zingine za leo ni Tottenham 3 West Ham 1, Southampton 2
Newcastle o huku Liverpool ikipata sare ya 0-0 kwa Swansea.
Via SALUTI 5 - www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment