EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, November 19, 2012

JK: Amfariji Paroko Aliyejeruhiwa Kwa Risasi Iringa.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Mhe.Wiliam Lukuvi akimfariji Paroko Angelo Burgeo (60) wa parokia ya Isimani Iringa aliyelazwa Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa kwa risasi na majambazi
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera na uratibu wa bunge ,Wiliam Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani akimfariji msaidizi paroko wa Parokia ya Isimani Herman Myalla (36) wa Kanisa aliyelazwa Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuvamiwa na majambazi juzi

Na :  Francis Godwin
KUFUATIA kuvamiwa kwa makanisa matatu mkoani Iringa na kujeruhiwa kwa paroko wa parokia ya Ismani mkoani Iringa Rais Dkt Jakaya Kikwete amfariji huyo paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) waliojeruhiwa na majambazi huku akiziomba taasisi za dini kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yao kama njia ya kukomesha matukio ya ujambazi yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za dini.

Rais Dkt Kikwete alitoa wito huo kupitia waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake walivamiwa ,alitoa wito huo leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa alipokuwa akiwasilisha salamu za Rais Jakaya Kikwete na kutoa pole kwa Paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa.
Novemba 15, mwaka huu mapadri hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu, walivamia na kushambuliwa kwa silaha za moto, mapanga na nondo na majambazi.
Watu watano wanaosikiliwa na polisi wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo ambalo mapadri hao mbali na kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni 3.8.
Akiwasilisha salamu za Rais, Lukuvi alisema ametumwa kutoa pole kwa wahanga hao, waumini na viongozi wa dhehebu hilo la dini kwa ujumla wake.
“Tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ambacho majambazi wamekuwa wakiwavamia viongozi wa dhehebu hili la dini wakiamini mmehifadhi fedha na mali nyingine nyingi ndani ya parokia zenu,” alisema.
Alisema tukio la mapadri hao kuvamiwa na kujeruhiwa mkoani Iringa limekuja miezi michache baada ya matukio kama hayo kutokea katika parokia za Migori na Pawaga mkoani Iringa.
“Serikali imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa mgambo wengi karibu katika kila kijiji, ni wajibu wa taasisi hizi za dini kuwatumia hao au vinginevyo ikubali kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa walinzi wao,” alisema.
Akipokea salamu hizo, Padro Burgeo alisema majambazi hao walifanikiwa kuingia ndani ya parokia yake baada ya kutumia lango la nyuma na kufanikiwa kuwapiga chenga walinzi wao.
Alisema katika tukio hilo ilikuwa afe lakini Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake baada ya kufikishwa mikononi mwa madaktari.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Faustine Gwanchele alisema baada ya kumfanyia upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri Burgeo hali yake inaendelea vizuri pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate