Papa Benedict amewatawaza makadinali sita wepya, kwenye sherehe iliyofanywa Vatikani.
Mwandishi wa BBC alioko Vatikani, anasema
makadinali hao wameteuliwa baada ya malalamiko kutoka viongozi wa kanisa
la Katoliki katika nchi zinazoendelea, kwamba makadinali walioteuliwa
awali mwaka huu walikuwa wengi wazungu, hasa Wataliana wanaotumika
Vatikani.
Kwa mara ya kwanza hakuna mzungu wala Mtaliana kati ya makadinali wepya.
Lakini wazungu ndio wengi ndani ya baraza kuu la makadinali 120 ambalo ndilo humchagua papa mpya.
Mtindo unaelekea kuwa na kanisa litalowakilisha wafuasi wake ulimwenguni.
Papa aliwakumbusha makadinali wepya kwamba kofia
na makoti mekundu wanayovaa ni alama kuwa wamejitolea kumwaga damu
kutetea imani yao ikihitajika.
Papa Benedict piya alisisitiza kuwa Kanisa Katoliki ni la binaadamu wote wa utamaduni na makabila yote.
Uamuzi wa Papa wa kuteua makadinali kutoka nchi
tatu zenye Waislamu wengi, yaani Libnan, Nigeria na India, unaonesha ana
wasiwasi juu ya uhusiano baina ya Ukristo na Uislamu.
Kadinali kutoka Libnan ni kasisi wa kati ya makanisa kongwe kabisa Mashariki ya Kati.
Askofu wa Abuja, kadinali mpya kutoka Nigeria
ambako nusu ya wananchi ni Waislamu, anaweza pengine siku moja kuwa papa
wa kwanza kutoka Afrika.
Via BBC SWAHILI
Via BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment