Taarifa ya habari ya Star tv ya saa mbili usiku ya tarehe 23/11/2012 imeeleza kuwa wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wanadaiwa kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma.
Habari hii inasikitisha hasa ukizingatia umuhimu wa wasomi hawa katika Tanzania na hatari inayoweza kuwapata kama taarifa hii ina ukweli.
Kama jamii tujiulize, tatizo ni nini mpaka mtu wa level kama hiyo kuamua kuvaa vichupi na kujiuza kwenye clubs na sehemu zingine??
CHUO KIKUU cha Dodoma UDOM kinadaiwa kukumbwa na kashfa ya ngono kufuatia madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za kwanza,uzamili na shahada za uzamivu.
Chuo Kikuucha Dodoma ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia sifa kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni pa wengi.
Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza.
Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment