Marehemu
Mary Shabani Kachua (3 Yrs) enzi za uhai wake.
Familia
ya Dr Shabani Kachua kutoka Canada inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao
mpendwa Mary Kachua kilichotokea tarehe 19/11/2012 nchini Canada.
Mwili
wake uliagwa jana York Funeral Home, Fredericton, NB. Canada na leo kutakuwa na
misa maalum Symthe Cathedral Church, Fredericton, NB, Canada.
Familia
ya Dr S. Kachua wataondoka leo Canada kuelekea Jijini Dar es salaam Tanzania
kwa ajili ya kuupokea mwili na wanatarajiwa kufika kesho jumapili saa 7:30
Mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines.
Mwili
wa marehemu Mary Kachua unatarajiwa kufika siku ya Jumatano tarehe 28/11/2012
kwa ndege ya KLM. Shughuli na taratibu za mazishi zinatarajiwa kufanyika
nyumbani Tanga mjini.
Kwa
mawasiliano zaidi ya taratibu zote za mazishi unaweza ukapiga namba:
+255
784 670866
+255
713 254553
Mwenyezi
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.
Amen
Chanzo cha habari na josephatlukaza.blogspot.com
No comments:
Post a Comment