EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, November 18, 2012

TGNP Yavipongeza Vyombo vya Habari.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo
Mmoja wa maofisa wa TGNP kutoka Idara ya Habari na Mawasiliano, Deo Temba (kushoto) akichukua kumbukumbu katika mkutano huo na wahariri. Pembeni yake ni Prof. Ruth Meena
Mmoja wa wahariri kutoka vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jane Mihanji na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) akichangia mada katika mkutano
Mwandishi wa habari na mmiliki wa Francis Godwin Blog akiwa katika mkutano huo
Prof. Meena (kulia) akifafanua jambo
Prof. Meena Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGNP, Profesa Ruth Meena pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Mary Nsemwa.

Na Mwandishi wa Thehabari.com

KAIMU Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mary Nsemwa amevipongeza vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa kile sasa kutoa nafasi ya kuridhisha kwa kuandika masuala mbalimbali ya kijinsia ambayo hapo awali yalikuwa hayapewi nafasi ya kutosha.

Bi. Nsemwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari katika mkutano wao na TGNP, kuzungumzia changamoto anuai za kijinsia na vyombo vya habari pamoja na ushiriki wa wanawake katika mchakato wa maoni ya uundwaji wa katiba mpya.

Alisema ushirikiano mzuri uliojengeka kati ya taasisi hiyo na vyombo vya habari umesaidia kwa kiasi kikubwa hivyo masuala ya kijinsia na hasa yale yanaowakandamiza wanawake kusikika katika vyombo vya habari hali ambayo imesaidia kwa kiasi fulani.

“…Tumejifunza mengi kutoka katika vyombo vya habari, vyombo hivi sasa vimewaunganisha wanawake…sauti za wasiosikisa hasa wa vijijini sasa zinasikika kupitia vyombo hivi. Vyombo vya habari pia vimepaza sauti kwa kampeni yetu ya Haki ya Uchumi; ‘Rasilimali Ziwanufaishe Wanawake walioko Pembezoni’ na mkumbuke kwamba nyinyi mnanguvu zaidi yetu,” alisema Bi. Nsemwa.

Naye mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Profesa Ruth Meena akiwasilisha mada katika mkutano huo wa wahariri alisema mambo mengi ya msingi ambayo ni miongoni mwa madai ya wananchi yameainishwa katika Katiba iliyopo sasa, hivyo kushauri ipo haja ya kuangalia namna ya usimamizi wa sheria na mabadiliko kadhaa kuingizwa kwenye Katiba Mpya.

“...Kwa upande mmoja  Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa haki sawa kwa wanawake na wanaume katika nyanja za siasa, uchumi na ustawi wa jamii, na hapohapo  kuzipokonya kwa mkono mwingine kwa kuruhusu kuendelezwa kwa sheria, taratibu na tabia zinazokinzana na katiba,” alisema Prof. Meena.
Aidha alishauri Katiba mpya ibatilishe sheria zote zinazokinzana na haki za msingi za wanawake na watoto wa kike hususani kubatilisha sheria na mila zote za ubaguzi wa jinsia, ubaguzi dhidi ya watoto hususani watoto wa kike, katika maswala ya ndoa, mirathi, haki za kumiliki. 
“Kwa mantiki hii, katiba ibainishe kwa uwazi haki za wanawake na haki za watoto. Pamoja na kuwajibisha serikali kuchukua hatua zote za kisera na sheria ili kulinda na kuhifadhi haki za wanawake na za watoto katika maeneo hayo, na pia iwajibishe serikali kutekeleza mikataba yote iliyoridhia kuhusu haki za wanawake ( CEDAW, CRC, ILO Conventon) Mikataba hii itambulike kuwa ni sheria za nchi  ili kuepusha ucheleweshaji wa kutafsri au kuruhusu uchakachuaji wamikataba hii katika sheria za nchi,” alifafanua Prof. Meena.
Pamoja na hayo alishauri Katiba mpya iangalie haki ya ufikiaji wa huduma za jamii; haki ya kufikia na kufaidi  huduma za msingi kama vile maji, chakula, malazi na elimu na hifadhi ya jamii ziendelee kuwepo - pamoja na kusisitiza wajibu wa serikali wa kuhakikisha huduma hizi za msingi zifikiwe  na ke na me ( rika zote, na hali zote).
-Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate