UJINGA wa Emmanuel
Adebayor umesababisha Tottenham kula kipigo cha mwaka 5-2 kutoka kwa
Arsenal katika mechi ya kuvutia ya London derby kwenye Uwanja wa
Emirates.Adebayor alifunga dhidi ya waajiri wake wa zamani bao la dakika ya 10 lakini dakika saba baadaye wakati alipewa nyekundu kwa kumfanyia rafu mbaya Santi Cazorla.
Tottenham
ilijitahidi kukabiliana na hasara ya kuwa pungufu lakini ni Arsenal
waliozawazisha muda mfupi baadae kupitia kwa beki wake Mertesacker.
Bao
la Lukas Podolski dakika ya 42, na Olivier Giroud (dak 45) likiwa ni
bao lake la tano katika michezo yake mitano iliyopita zilipeleka Arsenal
mapumziko kwa starehe ya tofauti ya bao 2.
Tottenham
ilifanya maboresho nusu ya pili, lakini ni Arseno waliopata bao la nne
kupitia kwa Santi Cazorla dakika ya 60 kabla Gareth Bale kufungia
Tottenham bao la pili dakika ya 71.
Kutia chumvi kwenye kidonda, Theo Walcott tulistahili akacheka na nyavu dakika za wa majeruhi kufanya mabao yasomeke 5-2.
Katika
mechi zingine zilizovuta hisia za wengi ni ile iliyoshuhudia Chelsea
ikilala 2-1 dhidi ya West Brom pamoja na ile ya Manchester City
iliyovuna ushindi mkubwa wa 5-0 kwa Aston Villa magoli ya David Villa,
Aguero (2) na Tevez (2) huku Liverpool ikiitandika Wigan 3-0 mabao
mawili yakitokea kwa Luis Suarez
Ushindi
wa Arsenal ina maana wao wanaruka juu ya Tottenham katika msimamo wa
ligi, huku kocha wa Tottenham Andre Villas-Boaz, akiwa na maswali mazito
ya kwenda kujibu kujibu kuhusu kwa nini aliamua kumchezesha Adebayor iwapo kulikuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wa mshambuliaji kudhibiti hisia zake.Via Saluti5.
No comments:
Post a Comment