BONGO MOVIE WAJIPANGA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA.
Bongo Movie inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake ambao
wataweza kuliongoza gurudumu la filamu kusonga mbele zaidi kutokana na
kuwepo na taarifa kuwa viongozi waliopo ni wabinafsi na wanajinufaisha
wenyewe.Kwa mujibu wa katiba ya Bongo Movie viongozi hukaa madarakani kwa
mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mpya ambapo viongozi waliopita huruhusiwa
kugombea tena.
“Kwanza sisi tuna katiba yetu ambayo inaendesha klabu yetu kwahiyo
katiba yetu moja ya vipengele ni namna ya uchaguzi, uongozi unakaa
madarakani kwa muda wa mwaka mmoja kwahiyo inapofika lazima sheria
ifuatwa ndio maana tunafanya uchaguzi mwishoni mwa mwezi huu na kikao
cha kujadili uchaguzi huo utafanyia wapi tutajadili Jumanne tarehe 20
wiki ijayo, “mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Bongo Movie ya uchaguzi
Jimmy mafufu
“Viongozi ambao wapo madarakani, mwenyekiti alikuwa JB, makamu wake
Athumani Mbilinyi, katibu ni Claud na Jackline Wolper lakini mweka
hazina ni Richie Richie na Vicent Kigosi alikuwa ni msaidizi wake,
lakini hii haimaanishi kwamba wanatoka, wanarusiwa tena kugombea wala
katiba haiwafungi,”aliongeza.
“Nashukuru Mungu kwasababu wamechukua hizo form na kwa yoyote mwenye
kuHitaji form ya uongozi anaweza akawasiliana na Bongo Movie ili apate
form ya uongozi.”
No comments:
Post a Comment