DORIS MALIYAGA WA MWANASPORT.
UWANJA wa kufa mtu unashushwa na Wachina Jangwani. Yanga inajenga uwanja wa kisasa ambao utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 40,000 ikiwa na maana kuwa inazidiwa na timu chache za England kwa kuwa na uwanja unaobeba mashabiki wengi.
Uwanja huo utauzidi uwanja wa White Hart Lane unaotumiwa na Tottenham Hotspurs ya London unaobeba mashabiki 36,230. Uwanja wa huo ulijengwa mwaka 1899.
Uwanja wa Yanga ukikamilika utauzidi Uwanja wa Tottenham kwa idadi ya mashabiki 3,770 jambo ambalo litakuwa ni historia kwa klabu hiyo ya Jangwani iliyoanzishwa mwaka 1935.
Viwanja ambavyo vinauzidi uwanja wa Yanga kwa England, vitakuwa ni Old Trafford (Manchester United), Emirates (Arsenal), St James' Park (Newcastle), Stamford Bridge (Chelsea) na Anfield (Liverpool).
Uongozi wa Yanga umesema unaanza harakati za ujenzi wa uwanja mpya eneo uliopo Uwanja wa Kaunda.
Uwanja huo utajengwa kwa nguvu za wanachama wa klabu hiyo na unatarajiwa kukamilika baada ya miaka miwili.
Utakapomilika, unatarajiwa kuchukua watazamaji kati ya 30,000 na 40,000 huku ukiwa na hoteli pia. Uwanja huo utajengwa na Kampuni ya Beijing Construction.
Makubaliano ya ujenzi huo yameanza hatua ya awali katika kuubuni na utafiti ili kufahamu gharama zitakazotumika na baada ya hapo wataingia nao mkataba rasmi wa ujenzi ambao unatarajiwa kuanza rasmi Juni mwakani.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema: "Shughuli za ujenzi zitaanza sasa, lakini kwa hatua ya awali lazima tufahamu gharama na mambo mengine baada ya hapo tutaingia mkataba rasmi wa ujenzi.
"Ieleweke kuwa ujenzi wa uwanja huo hautajengwa kwa nguvu ya mtu mmoja bali wanachama wenyewe wa Yanga, tutaangalia itakavyokuwa katika kuchangishana ili kila kitu kiende sawa," alisema Sanga.
"Lakini pia ipo njia nyingine ya pili ya kupata pesa kupitia mkopo ambao hautategemea dhamana ya jengo hili, tutaangalia itakavyokuwa na malipo yanaweza kufanyika kupitia malipo ya uwanjani au vinginevyo," alifafanua.
Kiongozi huyo alisema lengo la mpango huo ni kuongeza uchumi wa klabu hiyo na kuepuka gharama nyingine kama wanavyotumia Uwanja wa Taifa wenye makato mengi ambayo kwao itakuwa tofauti.
Naye meneja wa Beijing Construction, David Zhang alisema: "Tumefurahi kuingia katika historia ya ujenzi wa uwanja huo kwani ni historia."

No comments:
Post a Comment