Sonali Mukherjee akiwa kwenye kipindi maarufu cha ‘Who want to be a Millionaire’ kinachorushwa kwenye televisheni za India sambamba na Lara Dutta na Muongozaji wa Kipindi hicho Amitabh Bachchan al maarufu kama Big B.

 Sonali Mukherjee anavyoonekana hivi sasa baada ya kumwagiwa tindikali.
Sonali ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 27 anayetoka katika jiji la New Delhi sasa ataweza kulipia awamu nyingine ya upasuaji baada ya kushinda zawadi ya juu kabisa ya kipindi ‘Who Wants to be a Millionaire’ kinachoendeshwa nchini humo.
Mwadada huyo aliyeshambuliwa na mtu aliyekuwa na rafiki zake, ameshinda Rupia Laki 25 sawa na takriban paundi 30,000 wakati alipoonekana katika hicho cha televisheni akiwa muigizaji maarufu wa India aliyewahi kuwa ‘Miss Universe’ Lara Dutta.
 Sonali Mukherjee kabla hajamwagiwa tindikali.
Muongozaji wa kipindi hicho cha luninga Amitabh Bachchan maarufu kwa Jina la Big B nchini India amempongeza Sonali kwa kujitokeza katika kipindi hicho.

Sonali Mukherjee akiwa kwenye msongo wa mawazo.