MKAZI wa Kata ya Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu,
Paul Sanungu ametaka katiba Mpya ifute mwenge wa uhuru kwani unalipa
taifa hasara.
Kwa upande wake Martin James mkazi wa kata hiyo, alisema katika Katiba Mpya asasi za kiraia na waandishi wa habari, watambuliwe kuwa ni mhimili wa nne wa dola.
Alisema pia kuwa tume ya Nyalali ilipendekeza sheria 40 kandamizi ambazo mpaka sasa zimesahaulika, hivyo Katiba Mpya ihakikishe mapendekezo hayo yanafanyiwa kazi.
Alieleza pia kuwa sheria ya ardhi ya mwaka 2009, inayosema mtu akikaa sehemu kwa muda wa miaka 12 ardhi hiyo ni yake, ifutwe.
“Mtu umemkaribisha ili ajitafutie maisha sasa akikaa miaka 12 anakwambia ardhi ni yake, inatakiwa hiyo sheria ifutwe,” alisema.
No comments:
Post a Comment