HARAKATI za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye za kuhakikisha kwamba anaimaliza Chadema pamoja na Katibu Mkuu wake Dr Willibrod Slaa zimemtokea puani na kulazimika kutoa ufafanuzi wenye lengo la kuomba radhi kwa kile alichokisema dhiti ya Dk Slaa kuwa anakadi ya CCM na bado anaendelea kuilipia hadi hivi sasa.
Katika maelezo ya Nape yaliyoanza kudailiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii hususan mtandao wa Facebook Nape alionyesha ni jinsi gani jitihada zake za kutaka kumchafua na kummaliza kisiasa Dk Slaa zimegonga mwamba huku Chadema pamoja na
Dk Slaa wakiendelea kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi wowote juu ya suala hilo huku pia kukiwa na mijadala mingi ya kumsema Nape kwa madai yake hayo.
Hata hivyo baadhi ya wachangia wa hoja hiyo walisema kwamba watu
wanaoendelea kumponda nape wamesahau kwamba Nape ni kiongozi wa chama
wala sio wa serikali...hivyo anayo haki ya kukosoa, kushindana juu ya
kitu chochote kwenye mizani za kisiasa.
Mtoa hoja huyo alidai kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kuendelea
kumsakama Nape matusi mengi ni kuendelea kueneza waraka huo wa Dk Slaa
kumiliki Kadi ya CCM na kukifanya CHADEMA kutumia nguvu kubwa ya za
kujaribu kuzuia kuenea kwa habari hizo, kwamba hali itazidi kuwa imekuwa
tofauti kwani kila kukicha mjadala wa kadi ya Dk Slaa ndiyo itazidi
kuibuka huku Chadama wenyewe pamoja na Katibu Mkuu wake huyo wakishindwa
kutoa tamko lolote juu ya madai hayo ya Nepe.
Hata hivyo Nape Mwenyewe katika utetezi wake baada ya kuona mambo yamezidi kumgeukiwa alisema kwamba, "Nazitambua juhudi za wafuasi wa babu na mashabiki wake katika kujaribu kumtetea ionekane ni jambo la kawaida sana kwa yeye babu( Dr. W. Slaa) kuwa na kadi ya CCM mpaka leo! Juhudi za kutumia social media na magazeti mengine hasa gazeti la M4C(TanzaniaDaima) kujaribu kumtetea babu na wakati huo kunikejeli na kunitukana japo kuwa kwa matusi ambayo lazima nikiri si mapya, yalishawahi kutumiwa dhidi yangu au watu wengine duniani. Hapa nitajibu hoja moja baada ya nyingine( wenye matusi mapya wanakaribishwa wakijisikia kunitukana tena)"alisema Nape.
Nape alifafanua kuwa "katika matamshi yangu hakuna mahali
nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu
kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwasababu ndogo
sana..kukairishwa lazima kumtukana Nape hata bila kupima kwa makini
hoja....nilichosema Dr. Slaa na baadhi ya vigogo wa CDM wana kadi za CCM
na baadhi yao wanazilipia mpaka leo. Sijazungumzia uanachama
wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukisha kuwa mwanachama wa chama
kingine uanachama wako CCM unakufa hapohapo.
Ni kweli kuwa hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kuwa na kadi
ya CCM kwa babu na maendeleo ya wananchi masikini, lakini babu anatafuta
kuwa kiongozi wa nchi ANAPASWA KUISHI YALE ANAYOYASEMA NA KUWA
MWAMINIFU KWA NAFSI YAKE MWENYEWE. Ni Dr. huyu ambaye huhamasisha
wananchi wengine warudishe kadi za CCM anapofanya mikutano ya hadhara
wakati yeye kabaki nayo bila kuanza yeye kuongoza kwa kuonyesha njia kwa
kuirudisha yake kwanza...USIPOKUWA MWAMINIFU KWA KIDOGO HUWEZI KUWA
MWAMINIFU KWA KIKUBWA PIA....si ajabu alishindwa kutii kiapo chako na
nadhiri yake kwa Mungu aliyoapa akiwa padri..leo nitashangaa akiwa
mwaminifu kwa binadamu mwenzake kama kashindwa kumweshimu Mungu".
Hata hivyo hakuishia hapo bali aliendelea kufafanua kuwa siku chache
sana zimepita babu aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema Kigamboni
kuwa ni mapandikizi ya CCM kwa chama chake...nikashangaa sana, babu
anawatuhumu wenzake ambao hawana hata kadi za CCM kama yeye kuwa ni
mapandikizi ya CCM huku yeye ambaye kwa tafsiri hii ni pandikizi namba
moja akijifanya ni msafi sana..nilichofanya ni kumkumbusha kuwa yeye
ndio "pandikizi" namba moja kwahiyo aanze kujifukuza yeye.Via www.habarimpya.com
No comments:
Post a Comment