Christiano Ronaldo atarejea na mabingwa mara tisa wa Champions League
Real Madrid katika uwanja wa Old Traford kupambana na Manchester United
ambako alijitokeza kuwa mshambuliaji hatari kabisa duniani.
Bayern Munich , ambayo ilifanikiwa kuingia katika fainali ya michuano
hiyo msimu uliopita na kuambulia patupu dhidi ya Chelsea , London,
inapambana mara hii na Arsenal London na Juventus Turin inatiana kifuani
na Celtic Glasgow. Paris St Germain ambayo imetumia fedha nyingi msimu
huu kununua wachezaji inakabiliana na Valencia ya Uhispania.
Real Madrid , mabingwa wa sasa wa Uhispania , wamekuwa katika hali ya kukatisha tamaa katika ligi ya nchi hiyo msimu huu na wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili katika kundi lao na mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund katika Champions League.
Lakini Ronaldo, mchezaji wa Manchester United kuanzia mwaka 2003 hadi 2009, atakuwa na hamasa kwa Real kufanya vizuri dhidi ya klabu ambayo alishinda medali ya dhahabu katika ubingwa wa Ulaya mwaka 2008.
Kocha wa Real Madrid , Jose Mourinho, ambaye aliwahi kuifunza Chelsea, pia atapambana na hasimu wake wa zamani Alex Ferguson.
"Nafikiri mashabiki watafurahi sana katika pambano hili la kufurahisha.
"Itakuwa kitu cha kufurahisha kwa kila mtu. Ningependa kucheza dhidi ya Manchester United katika sehemu za mwishoni mwa msimu huu wa champions league , lakini mashabiki wasingefurahi hata hivyo."
Manchester United mabingwa wa kombe hilo mara tatu, wamecheza na Real Madrid mara nane na kushinda mara mbili tu. Real , ambayo itaikaribisha Manchester katika mchezo wa kwanza Februari 13, iliweza kushinda mara ya mwisho kombe la Champions League mwaka 2002.
Barcelona inatisha
Barcelona hivi sasa wanapewa nafasi ya juu kulinyakua kombe hilo, licha ya kuwa wasingependa kukutana na timu yenye uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya kama mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan.
Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi amepachika wavuni mabao 90 mwaka huu wa 2012 na ameiiwezesha Barcelona kuongoza ligi ya Uhispania kwa points tisa sasa kutoka timu inayofuatia wakati Milan wako points 14 nyuma ya Juventus Turin inayoongoza ligi ya Italia , Serie A.
Bayern Munich timu iliyonyang'anywa tonge kinywani nyumbani na Chelsea
msimu uliopita inaongoza kwa points tisa katika ligi ya Ujerumani ,
Bundesliga. Bayern imefurahi kupangwa na Arsenal ikifahamu kuwa
wapinzani wao hao wanahangaika kujiweka sawa katika ligi ya Uingereza
Premier League.
Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund hawajisikii nafuu kukumbana na mabingwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk. Mwenyekiti wa Dortmund Hans Joachim Watzke amesema haikuwa timu ambayo tungependa kukumbana nayo wakati huu. Ni timu ngumu sana lakini tumeonyesha katika mtoano katika makundi kuwa tunaweza kushinda hata timu ngumu.
Mchezaji wa Bayern München Bastian Schweinsteiger akitokwa na machozi baada ya mchezo na Chelsea
Lakini majaliwa ya vigogo viwili vya soka la Hispania katika upangaji wa
timu zitakavyoshindana leo Alhamis katika makao makuu ya shirikisho la
soka barani Ulaya UEFA , umewavutia wapenzi wengi wa soka na wote
wamepambanishwa dhidi ya vilabu vikongwe vyenye uzoefu mkubwa katika
soka la Ulaya.Real Madrid , mabingwa wa sasa wa Uhispania , wamekuwa katika hali ya kukatisha tamaa katika ligi ya nchi hiyo msimu huu na wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili katika kundi lao na mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund katika Champions League.
Kocha Jose Mourinho katika mazoezi ya Real Madrid
Ronaldo kurejea Old TrafordLakini Ronaldo, mchezaji wa Manchester United kuanzia mwaka 2003 hadi 2009, atakuwa na hamasa kwa Real kufanya vizuri dhidi ya klabu ambayo alishinda medali ya dhahabu katika ubingwa wa Ulaya mwaka 2008.
Kocha wa Real Madrid , Jose Mourinho, ambaye aliwahi kuifunza Chelsea, pia atapambana na hasimu wake wa zamani Alex Ferguson.
Mchezo wa kundi D katika ya Real na Dortmund
"Nina hakika litakuwa pambano la pekee kwa Ronaldo" amesema Emilio
Butragueno, mkurugenzi wa Real Madrid anayehusika na mahusiano ya
taasisi."Nafikiri mashabiki watafurahi sana katika pambano hili la kufurahisha.
"Itakuwa kitu cha kufurahisha kwa kila mtu. Ningependa kucheza dhidi ya Manchester United katika sehemu za mwishoni mwa msimu huu wa champions league , lakini mashabiki wasingefurahi hata hivyo."
Manchester United mabingwa wa kombe hilo mara tatu, wamecheza na Real Madrid mara nane na kushinda mara mbili tu. Real , ambayo itaikaribisha Manchester katika mchezo wa kwanza Februari 13, iliweza kushinda mara ya mwisho kombe la Champions League mwaka 2002.
Barcelona inatisha
Barcelona hivi sasa wanapewa nafasi ya juu kulinyakua kombe hilo, licha ya kuwa wasingependa kukutana na timu yenye uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya kama mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan.
Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi amepachika wavuni mabao 90 mwaka huu wa 2012 na ameiiwezesha Barcelona kuongoza ligi ya Uhispania kwa points tisa sasa kutoka timu inayofuatia wakati Milan wako points 14 nyuma ya Juventus Turin inayoongoza ligi ya Italia , Serie A.
Messi akichanja mbuga katika mpambano na Celtic
Mabingwa wa Ujerumani Borussia Dortmund hawajisikii nafuu kukumbana na mabingwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk. Mwenyekiti wa Dortmund Hans Joachim Watzke amesema haikuwa timu ambayo tungependa kukumbana nayo wakati huu. Ni timu ngumu sana lakini tumeonyesha katika mtoano katika makundi kuwa tunaweza kushinda hata timu ngumu.
Kikosi cha BVB Borussia Dortmund wakirejea baada ya kuweka mpira wavuni kwa Man City
Schalke 04 imepangwa dhidi ya Galatasaray ya Uturuki na Porto ya Ureno inapambana na Malaga ya Uhispania.
No comments:
Post a Comment