HABARI
za uhakika kutoka chini ya zulia zemesema kuwa nyimbo za msanii nyota
Naseeb Abdul (Diamond) zimepigwa marufuku kwenye kituo cha redio Magic
FM na kwenye luninga ya Chanel 10.
Inaaminika
kuwa vituo hivyo ambayo viko chini ya Africa Media Group, vimefikia
hatua hiyo baada ya kupishana na lugha na msanii huyo mwenye mafanikio
lukuki.
Kwa
zaidi ya miezi miwili sasa nyimbo za msanii zimekuwa hazionekani wala
kusikika kwenye vituo hivyo na hali hiyo imekwenda mbali zaidi ambapo
sasa hata nyimbo za wasanii wengine waliomshirikisha Diamond nazo pia ni
marufuku vituoni humo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjL_PQ8JdEkgjYz98z2WzMiPwHFr_omIISUx6R9iXnug3wdYHnUzGw2wEeUSwZUQkDgH_ZvjQpRCZ5oGbVc-9Hg3YaKIgJuWjBPt2MjaIHtsC5CPY3Ttea4rAuDwFkC22VFwjkLjRx8ong/s640/Naseeb-Abdul-alias-Diamond-Platnumz.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjL_PQ8JdEkgjYz98z2WzMiPwHFr_omIISUx6R9iXnug3wdYHnUzGw2wEeUSwZUQkDgH_ZvjQpRCZ5oGbVc-9Hg3YaKIgJuWjBPt2MjaIHtsC5CPY3Ttea4rAuDwFkC22VFwjkLjRx8ong/s640/Naseeb-Abdul-alias-Diamond-Platnumz.jpg)
Mmoja
wa wafanyakazi wa Magic FM ambaye hakutaka kutajwa jina kwa vile yeye
sio msemaji, aliiambia Saluti5 kuwa kuna bifu zito kati ya Diamond na
vituo hivyo lakini tayari mazunguzo ya kusafisha hali ya hewa yameanza
kufanyika.
Mtangazaji
huyo amsema Diamond pia ana matatizo na kituo cha televishieni cha DTV
ambacho nacho hakipigi nyimbo za msanii huyo na juzi Jumatano Diamond
alifika katika ofisi za Entertainment Masters (EML) ambao ndio wamiliki
wa DTV kwa ajili ya kikao cha kuweka mambo sawa.
Hatua
ya msanii huyo kwenda EML ilikuja baada ya wimbo alioshirikishwa na
Dully Sykes “Utamu” kupigwa chini na DTV kutokana na bifu lililopo kati
yake (Diamond) na wafanyakazi wa kituo hicho.Via saluti5.
No comments:
Post a Comment