Chelsea imeiangushia kipigo kizito Aston Villa kwa kuicharaza magoli 8-0 katika mechi ya ligi kuu ya England, iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge, siku ya jana.Fernando Torres, ndiye aliyeanza kufungua karamu ya magoli kwa vijana wa Rafael Benitez, pale alipopachika bao katika dakika ya tatu ya mchezo.
Fernando Torres akitupia goli la kwanza nyavuni
David Luiz kiungo mahiri
aliongeza goli la pili katika dakika ya 29 huku Branislav Ivanovic
akishindilia goli la tatu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.Frank Lampard alifungua kipindi cha pili kwa bao lake la dakika ya 58 huku Ramires akifunga magoli mawili, na mengineyakifungwa na Oscar, Eden na Hazard wakifunga kila mmoja goli moja moja.
John Terry akifurahia na mwenzake ushindi huo mnono wa goli 8-0!!
Ushindi huo umezidi kuiimarisha Chelsea
katika nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England ikiwa na pointi 32 katika
mechi 17 ilizocheza.Soma ubaoni...
WAFUNGAJI:
-Torres Dakika ya 3
-Luiz 29
-Ivanovic 34
-Lampard 58
-Ramires 75 & 90
-Oscar 79 (Penati)
-Hazard 83
Mbali ya kufunga Goli hizo 8 Chelsea pia
walikosa Penati baada ya Chipukizi toka Brazil, Piazon, kuipiga na Kipa
Guzan kuipanchi.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Luiz, Lampard, Moses, Mata, Hazard, Torres
Akiba: Turnbull, Ramires, Oscar, Ferreira, Marin, Piazon, Ake.
Aston Villa: Guzan, Herd, Clark, Baker, Lowton, Bannan, Westwood, Lichaj, Weimann, Holman, Benteke
Akiba: Given, Ireland, El Ahmadi, Albrighton, Delph, Bowery, Bennett.
Refa: Phil Dowd
No comments:
Post a Comment