Katika mchezo mwingine uliochezwa Jumapili, vinara wa ligi hiyo Manchester United walitoka sare ya bao 1-1 na Swansea.
Patrice Evra aliifungia timu yake bao la
kuongoza katika dakika ya 16 kwa njia ya kichwa kufuatia kona
iliyochongwa na Robin van Persie.
Hata hivyo Michu aliisawazishia Swansea katika dakika ya 29.
Mpaka sasa Manchester United inaongoza ligi kuu
ya England ikiwa na pointi 43 katika michezo 18, ikifuatiwa na
Manchester City yenye pointi 39 na Arsenal imejikita katika nafasi ya
nne ikiwa na pointi 30.
Manchester United bado wapo kileleni mwa
Ligi Kuu England kwa Pointi 4 mbele ya Mahasimu wao Man City licha ya
leo kutoka sare ya Bao 1-1 na Swansea City Uwanjani Liberty.
Man United walitangulia kufunga kwa Bao
la kichwa la Patrice Evra kufuatia kona ya Robin van Persie katika
Dakika ya 16 lakini Swansea walisawazisha katika Dakika ya 29 kwa Bao la
Michu baada ya shuti la Jonathan De Guz kutemwa na Kipa De Gea na kutua
kirahisi miguuni mwa Michu.Jitihada za Jonathan De Guzman zikizaa matunda na Michu kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa united
Michu akishangilia mara baada ya kuisawazishia timu yako goli
Kipindi cha Pili Man United walikosa Bao
nyingi pamoja na mbili zilizogonga mwamba lakini tukio ambalo huenda
likaleta mjadala ni pale Robin van Persie alipofanyiwa faulo na Refa
kupiga Filimbi lakini Beki wa Swansea, Williams, akaupiga mpira kwa
nguvu na kumbabatiza kichwani Van Persie wakati akiwa amelala chini na
Van Persie akapandwa na jazba na kuanza kuvutana na Williams.
Refa Michael Oliver aliwapa Kadi za
Njano Wachezaji wote hao wawili lakini Sir Alex Ferguson ametaka FA
ichukue hatua zaidi kwa Williams ambae alidai angeweza kumvunja shingo
Van Persie.
Nemanja Vidic (kulia) akigombania mpira na Michu
Patrcie Evra (kati) akikatiza katikati ya madifender wawili wa SwanseaFerguson amelalamikia hiyo rafu na kutaka William kufungiwa.
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akifoka baada ya mchezaji wake Robin van Persie kuchezewa rafu mbaya.
VIKOSI:
Swansea:Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Dyer, Britton, Agustien, de Guzman, Routledge, Michu
Swansea:Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Dyer, Britton, Agustien, de Guzman, Routledge, Michu
Akiba: Tremmel, Graham, Monk, Shechter, Moore, Ki, Richards.
Man United: De Gea, Jones, Evans, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley, Young, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Giggs, Hernandez, Welbeck, Scholes, Fletcher, Buttner.
Refa: Michael Oliver
No comments:
Post a Comment