Mitandao kadhaa barani Afrika imechapisha habari za kutengenezwa kuhusu bingwa wa zamani wa ndozi za uzito wa juu, Mike Tyson kuwa amebadilisha jinsia yake. (Kutoka mwanaume na kuwa mwanamke).
Makala ya kwanza ilionekana kwenye tovuti ya vituko ya Uingereza, NewsBiscuit, mwishoni mwa Novemba.Via saluti5
Baada ya hapo habari hizo zikaibukia Zimbabwe kupitia gazeti la Standard Jumapili kabla ya kufuatiwa na tovuti ya SpyGhana ya nchini Ghana Jumanne hii.
NewsBiscuit imetamba kuwa tovuti yao ilitembelewa na wasomaji wengi kutoka Afrika kufutaia habari hizo kuandikwa sana na mitandao ya Afrika.
"Tulikuwa
na zaidi ya nusu ya wageni kutoka Afrika katika siku chache zilizopita
na tulitarajia hivyo kwa mwezi mzima," mwandishi wa vituko, John
O'Farrell kutoka NewsBiscuit aliiambia BBC.
Alisema hadithi imetazamwa kwa zaidi ya mara 50,000 katika siku chache zilizopita, ikiwa ni mara 20 zaidi ya mara ni kawaida.
Makala hiyo ilisema kuwa bondia huyo sasa atajulikana kama Michelle na kwamba alijisikia vizuri baada ya kufanyiwa operesheni iliyochukua masaa 16.
Tafiti
zinaonyesha kwamba nchini Zambia tovuti Zambia Watchdog iliandika
Jumatatu ikiwa na kichwa cha habari "Mike Tyson afanya mabadiliko ya
kijinsia katika upasuaji uliofanikiwa”. Lakini ‘link’ hiyo kwa sasa inasema ukurasa hauwezi kufunguka.
Mr O'Farrell anasema hadithi ya awali ilipelekwa katika bodi ya waandishi wa NewsBiscuit na baadae timu ya mtandao huo ikaweka picha juu yake na kuichapa katika ukurasa wao wa mbele Novemba 30.
“Hii si mara ya kwanza kwa makala NewsBiscuit kuchukuliwa kwa uzito wa juu barani Afrika” anasema.
Katika mwaka 2007, ilitengeneza hadithi ya kizushi kuhusu Rais wa zamani wa Ghana, John Kufor na kumletea mtafaruku kwa waandishi wa nchini mwake.
Habari
hii ya NewsBiscuit ambayo haina ukweli wowote, ikiwa imelengwa mahsusi
'kupasua' vichwa vya watu, imekuwa kama sikukuu ya wajinga kwa
Watanzania ambapo vyombo vingi vya habari pamoja na mitandao ya kijamii
viliingia mkenge na kuitumia habari hiyo.
Icheki hapo chini habari yenyewe ilivyokuwa
No comments:
Post a Comment