KIPIGO
cha mabao 3-2 kutoka kwa Manchester United, kimewafanya mashabiki wa
Manchester City kukosa uvumilivu na mmojawao kuamua kumpiga kwa sarafu
Rio Ferdinand.
Ferdinand
alionekana kutupiwa kitu kutoka kwa mashabiki wa City wakati
akishangilia bao la ushindi lilipachikwa dakika za maheruhi na Robin van
Persie.
Mbali
na kipigo hicho kilichomuacha akivuja damu usoni, beki huyo wa United
pia alijikuta kwenye hatari nyingine wakati shabiki mwingine wa City
alipoingia uwanjani na kuelekea alipokuwa nahodha huyo wa zamani wa
England kwa ghadhabu.
Shabiki huyo alizuiwa na kipa wa timu yake, Joe Hart.
Bosi
wa United, Alex Ferguson alisema: "Kilikuwa kitu kisichokubalika kwamba
shabiki amekimbilia uwanjani baada ya Rio kupigwa sarafu
jichoni...Mechi haikusatahili hilo. Sijui kama kama atashonnwa au
hapana.”Asante saluti 5 kwa habari hii.www,saluti5.com
No comments:
Post a Comment