MKURUGENZI
wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, ametetea Miss Tanzania wa
zamani, Wema Sepetu kuwa vyombo vya habari vinakuza machafu yake badala
ya kumuelimisha.
Akiongea
na kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, Jumamosi usiku, Lundega alisema
mambo anayofanya Wema yanakuzwa kwa vile tu ni Miss Tanzania, lakini
inawezekana wako watu wasiojulikana wenye mambo machafu kuliko Wema.
“Mi
nadhani badala ya kuanika kila baya linalofanywa na Wema, vyombo vya
habari na jamii kwa ujumla vingejaribu kumuelimisha badala ya
kumshambulia” alisema Lundenga.
Aidha
Lundenga alipoulizwa kama maadili ya dini yake ya Kiislam yanakubaliana
na kazi anayofanya, alikataa kujibu na kusema jibu lolote atakalotoa
linaweza likaleta taabu.
“Ieleweke
tu kuwa mimi ni Mwislam na najua vita kubwa huwa ni ya kuvaa bikini,
ambayo Miss Tanzania hawavai, sipendi kuongelea mambo ya dini zaidi ya
hapo” alisema Lundenga.Via saluti5.
No comments:
Post a Comment