EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, December 12, 2012

JK: Serikali kujenga Hospitali kubwa ya kisasa mwaka 2013.

RAIS Jakaya Kikwete amesema ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa ambayo itafanana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), utaanza Januari, 2013 katika eneo la Mloganzila, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Ujenzi huo wa hospitali hiyo unatokana na mkopo wa Dola za Marekani 60,000 milioni sawa na Sh96 bilioni ambazo Tanzania imepata kutoka Korea ya Kusini.Kikwete alisema hayo jana wakati akifungua majengo matatu ya hospitali za Mnazimmoja (Ilala), Sinza (Kinondoni) na Mbagala Rangitatu (Temeke).

Ujenzi wa majengo ya hospitali hizo yenye maabara za kisasa, vifaatiba na magari ya wagonjwa yamefadhiliwa na Korea Kusini kwa gharama ya Sh6.7 bilioni.Alisema Hospitali ya Mlonganzila itakuwa ikitoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi na kwamba kila mwaka itakuwa ikifundisha madaktari 12,000 kuanzia itakapokamilika Januari 2015.
“Chuo Kikuu cha Muhimbili kinatoa madaktari 5,000, Dodoma wanatoa madaktari 5,000, Mloganzila wakitoa 12,000 tutakuwa na madaktari 22,000 kwa mwaka,” alisema Kikwete.
Alisema ujenzi wa hospitali hiyo utasaidia kumaliza tatizo la madaktari linaloendelea kuwepo hapa nchini.

“Madaktari waliopo ni wachache wanazunguka kutoa huduma katika hospitali zaidi ya mbili kwa siku,” alisema.

Akitoa takwimu, Kikwete alisema nchi zilizoendelea daktari mmoja anahudumia wagonjwa 500 wakati Tanzania daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.
“Bado tuko mbali sana tunahitaji kukimbia wakati wenzetu wanatembea, tunapofikiria kujenga zaidi hospitali tunatakiwa tuendelee kusomesha ili kupata madaktari,” alisema Kikwete.

Akizungumzia hospitali za kisasa alizozifungua, Kikwete aliishukuru Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo na kutaka Halmashauri za Kinondoni, Ilala na Temeke kutenga fedha za kutosha kila mwaka ili kuvifanyia matengezo vifaa hivyo.
Alisema Serikali inaendelea na juhudi zake katika kuhakikisha kwamba huduma za afya zinafika jirani na wananchi.

Balozi wa Korea nchini, Chung II alisema , Serikali yake inathamini umuhimu wa afya katika juhudi za Tanzania katika kujiletea maendeleo.
Alisema wananchi wanapopata huduma za afya za uhakika huwasaidia kushiriki katika kazi mbalimbali na hivyo kujiimarisha kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alimwomba Kikwete kutenga Sh1.2 bilioni kwa ajili ya kuwafidia wananchi wa Mbagala Rangi tatu ili kupisha upanuzi wa hospitali hiyo.

“ Licha ya hospitali hii ya kisasa kujengwa na Wakorea bado imezungukwa kwa karibu na nyumba za watu, tunaomba fedha ili tuweze kuwalipa fidia wananchi hawa waweze kupisha upanuzi zaidi,” alisema Sadiki.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate