Upinzani nchini Ghana umethibitisha rasmi kuwa
utapinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo siku ya Ijumaa
na Jumamosi.Chama cha upinzani NPP kimesema kuwa kitakwenda
mahakamani kupinga uhalali wa Rais John Mahama. Pia kinasema kuwa
kitasusia vikao vya bunge.
John Mahama alishinda uchaguzi mkuu wa Ghana lakini upinzani unapinga matokeo ya uchaguzi huo. |
Mnamo siku ya Jumapili, tume ya
uchaguzi ilimtangaza bwana Mahama kama mshindi wa uchaguzi huo kwa
kushinda kwa asilimia hamsini na saba.Ushindi huu ulimtosheleza kuweza kukwepa duru ya
pili dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata asilimia arobaini
na saba ya kura.Waangalizi kwenye uchaguzi huo wanasema kuwa ulikuwa huru na wa haki.
Ghana imekuwa ikitolewa kama mfano wa nchi iliyokomaa kidemokrasia katika bara la Afrika.
Chanzo BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment