JAMHURI
Kihwelu “Julio” ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa mabingwa wa soka
Tanzania Bara, Simba Sports Club na anaanza kuionoa timu kesho asubuhi.Hata
hivyo nafasi halisi ya Julio ni Meneja wa timu na kocha msaidizi,
lakini atakaimu nafasi ya ukocha mkuu hadi hapo kocha mkuu
atakapotangazwa rasmi.
“Simba sio timu mbaya, ila nimegundua kuwa stamina iko chini, nitamaliza tatizo hilo ndani ya muda mfupi” alisema Julio.
Julio
alisema: “ Wapenzi wa Simba wategemee makubwa, mimi ndio kocha wao,
nimeshazoea ingia toka katika Simba, lakini historia inajieleza wazi
kuwa kila ninapoingia Simba huwa ni neema tupu.
“Nina
mapenzi na Simba na nitafanya kazi kwa moyo mmoja sibabaishwi na mambo
yaliyotokea nyuma, kazi ya kocha siku zote ni mguu ndani mguu nje, kwa
mema au mabaya siku moja ni lazima utaondoka, lakini unaporudi unapaswa
kusahau yote yaliyopita” alisema Julio ambaye ana rekodi nzuri na Simba
kuanzia kwenye uchezaji hadi ukocha.Via saluti5.
No comments:
Post a Comment