Kocha huyo kutoka Ufaransa, amekuwa kwenye mgomo baridi baada ya FKF kutomlipa mshahara wake wote.
Aliyekuwa kocha wa Kenya
Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Ubalozi wa Ufaransa mjini Nairobi kocha huyo anarejea nyumbani.
Hata hivyo barua hiyo inaashirikia kuwa kocha
huyo alijiuzulu tarehe kumi mwezi huu lakini tangazo hilo limetolewa leo
tarehe 17 Desemba.
Michel alikataa kuongoza Harambee Stars wakati
wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika Mashariki
na Kati CECAFA, akiitaja mashindano hayo kama mashindano yasiyokuwa na
maana yoyote.
Aliyekuwa kocha wa Kenya Henri Mitchel
Kocha huyo alisema jukumu lake kuu ni
kuhakikisha Kenya imejianda vyema kwa michuano ya kuwania ubingwa wa
mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani.
Awali rais wa shirikisho la mchezo wa soka
nchini Kenya Sam Nyamweya alikariri kuwa kocha huyo alikuwa na jukumu la
kuandaa Harambee Stars kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka
wa 2014.
Michel aliongoza Harambee Stars katika mechi
mbili pekee. Katika mechi ya Kwanza Harambee stars ililazwa magoli 2-1
na Bafana Bafana ya Afrika Kusini mjini Nairobi na pia kulazwa 1-0 na
Kilimanjaro Stars ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment