Huku raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo wakiwa na matumaini ya
kupatikana amani nchini mwao kutokana na mazungumzo yanayofanyika nchini
Uganda, sasa inaonekana matarajio yao huenda yakazimika
Wakati raia wa Congo wakiendelea kutegea sikio yale yanayojitokeza
katika mazungumzo yanayoendelea
Kampala baina ya wajumbe wa serikali ya
jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23, mazungumzo hayo bado
yanaonekana kukabiliwa na mkwamo. Na ili kukwamua mazungumzo hayo,
msuluhishi kwenye mazungumzo hayo waziri wa ulinzi wa Uganda Dr Crypius
Kiyonga, yuko katika mchakato wakukutana na viongozi wa ujumbe wa M23,
ili pande zote husika zikubali kurudi kwenye meza ya majadiliano.Kwa mengi zaidi sikiliza ripoti ya mwandishi wetu John Kanyunyu aliyeko Kampala Uganda.
No comments:
Post a Comment