MENEJA
wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa hatajiuzulu
wadhfa huo pamoja na timu yake kufungwa mabao 3-2 na Malaga ambao
umewafanya kuachwa alama 16 na vinara wa La Liga Barcelona.
Kufungwa kwa Madrid kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho kufuatia
uamuzi wake wa kumuacha golikipa ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo Iker
Casillas katika kikosi cha kwanza. Akihojiwa kama anahofu kibarua chake
kitakuwa kimefikia ukingoni mara baada ya mchezo Mourinho amesema
hahofii chochote na hawezi kuachia ngazi kwani kupoteza mechi ni sehemu
ya mchezo la msingi ni kujipanga na kuangalia wapi walikosea.
Hiyo ni
mara ya kwanza kwa Casillas katika kipindi cha miaka 10 kupumzishwa
benchi na kumpisha golikipa namba mbili Antonio Adan mwenye umri wa
miaka 25.
No comments:
Post a Comment