Rais Barack Obama amemwonya rais wa Syria Bashar al-Assad kwamba
atawajibishwa endapo majeshi yake yatatumia silaha za kemikali dhidi ya
upinzani nchini Syria.
Bw. Obama alitamka hayo katika kikao hapa Washington kusisitiza msimamo wa Marekani dhidi ya ulimbikizaji wa silaha za nuklia na kemikali wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya mkataba wa ushirikiano wa kupunguza vitisho vya silaha za kemikali kati ya Marekani na Russia.

Lakini kilichogonga vichwa vya habari ni onyo lake kwa rais wa Syria,
siku moja baada ya Washington kuionya Damascus dhidi ya matumizi ya
silaha za kemikali. Bw. Obama alisema Marekani itaendelea kuunga mkono
azma halali ya raia wa Syria, na kutoa misaada ya kibinadamu kwa
upinzani na katika makabidhiano huru ya madaraka pasipo utawala wa
Assad.
Alimwonya rais Assad kuwa dunia inatizama kinachoendelea nchini Syria
na kwamba matumizi ya silaha za kemikali kamwe hayatakubalika. Na ikiwa
atafanya kosa la kutumia silaha hizo kutatokea madhara na Assad
atawajibika.
Bwana Obama alisisitiza kuwa dunia haiwezi kuruhusu karne ya 21 kutumbukizwa katika kiza cha karne ya 20 ya matumizi ya silaha kama hizo. Alisema jukumu la kuzuia ugaidi wa kutumia silaha za nuklia ni mojawapo ya maswala yaliyopewa kipaumbele kwa usalama wa kitaifa , na kwamba dunia inasogea mbele kuhakikisha hakuna silaha za nuklia katika siku za usoni.
No comments:
Post a Comment