MSANII wa filamu na tamthilia bongo Rayuu,
inadaiwa kuwa amenusurika kupelekwa polisi na mwanamke mmoja kwa madai
kuwa alikuwa akitembea na mume wake, huku pesa nyingi za matumizi
zilikuwa zikienda kwa msanii huyo.
Wiki iliyopita hali ilikuwa ngumu kwa msanii huyo kwani taarifa za kupelekwa polisi zilimpa wakati mgumu hadi kuchukua hatua ya kujifungia ndani ili kupumzika na kupisha taarifa hizo ambazo zingemchafua pengine hata kujiigiza kwenye matatizo makubwa.
Chanzo kimoja kilichozungumza kilidai kuwa msanii huyo alikuwa akitembea na jamaa huyo bila kujua ni mume wa mtu huku wakitanua sehemu tofauti tofauti za starehe.Hata hivyo taarifa hizo za kuonekana sehemu kadhaa na jamaa zilimfikia mke huyo anayedaiwa kuwa mke wa jamaa, ndipo alipotafuta namba ya simu ya Rayuu na kumtaka aachane na mume wake mara moja bila hivyo anaweza kumfikisha kituo cha polisi na akajibu mashtaka.
“Wiki iliyopita tu huyo mwanamke baada ya kupewa taarifa kuwa mume wake anakula bata na msanii huyo, ndipo alipoamua kuchukua maamuzi ya kumpigia simu Rayuu ili kumwambia achane na mume wake,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mwandishi alimtafuta Rayuu ili kuzungumzia ishu hiyo, ambapo alidai kuwa alipigiwa simu na mwanamke huyo ya kumtaka achane na mume wake, lakini awali kabisa hakujua kama ni mume wa mtu.
Alisema hakuwa na makosa kwani jamaa alipomfuata hakusema kuwa ni mume wa mtu na wala hakuwa na ishara zozote zinazoonesha ana mke nyumbani na muda wote alipomtafuta walikuwa wakionana na kufanya yote kama wapenzi.
“Sikujua kama ni mume wa mtu na nimekuwa naye katika mahusiano kwa muda mrefu lakini nilipatwa na mshtuko baada ya mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa jamaa huyo kunipigiwa simu tena kwa matusi na kudai kuwa nikae mbali na mume sikujua anazungumzia nini lakini baada ya muda jamaa mwenyewe akaniweka wazi kuwa ni mume wa mtu,” alisema Rayuu.
Alipoulizwa swali kuwa baada ya kujua jamaa ni mume wa mtu alichukua hatua gani, alidai kuwa hakuwa na kitu cha kufanya zaidi ya kuachana na jamaa kwani hataki yaje kumkuta makubwa zaidi.

No comments:
Post a Comment