Kundi moja la mashabiki wa soka
nchini Uingereza limesema kuwa vilabu kumi na vitatu nchini Uingereza
vimesemekana kuunga mkono, uamuzi wa kuruhusu mashabiki kutizama mechi
wakiwa wamesimama.
Mashabiki wa Soka wa Uingereza.
Kundi hilo linaamini kuwa mpango uliopigwa marufuku baada ya mkasa uliotokea katika uwanja wa Hillsborough mwaka wa 1989, sasa ni salama.
Awali wasimamizi wa ligi kuu ya Premier walisema kuwa hawataunga mkono pendekezo hilo.
Msemaji wa kundi hilo la FSF, Peter Daykin asema'' Tunahitaji kuchunguza ikiwa itafaulu na njia ya pekee ya kupata jibu ni kwa kuijaribu''
Mkasa wa Hillsborough
Tangu mwaka wa 1994, mamshabiki wote wa soka ni sharti waketi wakati mechi inapoendelea.
Eneo la kumbukumbu ya mkasa wa Hillsborough
Lakini mbunge mmoja Roger Godsiff amewasilisha mswada bungeni kutaka serikali kuidhinisha majaribio ya mpango huo.
Kundi la FSF limesema wazo hilo linaungwa mkono na klabu ya Aston Villa, timu zinazoshiriki katika ligi kuu ya Premier nchini Scotland, likiwemo ilabu ya Peterborough United, Cardiff City, Crystal Palace, Derby County na Hull City.
Mpango huo unapendekeza kuanzishwa kwa mfumo ambao mashabiki wataketi sawa na vile wanavyoketi kwenye treni, mfumo ambao kwa sasa unatumiwa katika mataifa kadhaa ya Ulaya kama vile Ujerumani.
Viti vitapangwam kwa njia fulani ili kuruhusu mashabiki wengine waketi chini na wengine wasimame.
Wataalamu wa soka akiwemo afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Aston Villa, paul Faulkner na mkuu wa idara ya polisi katika eneo la Midlands Steve Graham wanatarajiwa kuwasilisha suala hilo la kuruhusu mashabiki kusimama, mbele ya kamati maalum ya bunge hii leo.Via BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment