EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, December 11, 2012

TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU KWA KAULI MBIU YA “SAUTI YANGU INACHANGIA”.


Meza Kuu ikipokea maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu zilizofanyika jijini Dar leo.

Mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kusalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot.
Pichani Juu na Chini ni maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu yaliyohusisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali, Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu yakiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu ambapo aliwasilisha Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa nchi zote zihakikishe kuwa zinafuata maazimio ya tamko la haki za binadamu na wananchi wake wanufaike na haki zilizomo ndani yake.
Mwanasheria Mkuu wa Sreikali Jaji Frederick Werema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema chini ya mpango wa pamoja, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya serikali na wadau wengine wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya Asasi zisizo za kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu. Vilevile amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia ahadi zilizotolewa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mapendekezo yakiwemo kutoka katika Bodi za Mikataba ya haki za Binadamu.
Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Abdu Mohammed akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesisitiza kila raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki katika masuala ya umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa kuchaguliwa, pia kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza kufikia huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kuungana. Amongeza kuwa haki hizi zinatakiwa kumhusu kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye baguliwa kwa moja kati ya hizo kwa sababu ni mwanamke, au anatoka katika kundi dogo, au anaabudu katika dini Fulani, au kwa sababu ni shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au mkimbizi au ana rangi fulani, anatoka katika kabila Fulani.
Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.
Mh. Pinda amesema hatua ya kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii au Kitaifa.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) na Naibu wake Mh. Angellah Kairuki (kulia).
Sasa imezinduliwa rasmi....Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto).
Waziri Mkuu Pinda akipitia ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kikundi cha Wana wandime ya kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Pichani Juu na Chini ni Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali, Wanafunzi wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu na Wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu huku akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate