WAKULIMA wapatao 40,000 waishio katika vijiji 11 vilivyoko
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, hawana mahala pa
kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na uongozi wa halmashauri hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mwishoni mwa
wiki wakazi hao ambao wanadaiwa kuvamia hifadhi ya mbuga ya Embloy
Murtangosi, walisema wameonewa na kunyanyaswa kwa kuitwa wakimbizi
kutokana na baadhi ya vigogo wa serikali kulitaka eneo hilo la
hifadhi.Mmoja wa wakulima hao ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Leitimi, Majaliwa
Mbaigwa, alisema wao ni wakazi wa wilaya ya Kiteto
tangu mwaka 2003 na waliambiwa na halmashauri hiyo kusogea umbali wa
kilomita mbili tu na si vinginevyo.
Alisema wamekuwa wakifanya shughuli zao za kilimo na kulipa ushuru wa
halmashauri na kupatiwa risiti ikiwa ni pamoja na kuchangia shughuli za
maendeleo kama ujenzi wa barabara, lakini cha kushangaza wanaitwa
wakimbizi.
“Ajabu wameongeza eneo kutoka kilomita mbili hadi 20 na kutufanya sisi
tuonekane tumevamia, jambo ambalo si halali,” alisema Mbaigwa.
Naye Anna Ngamia ambaye alikuwa akizungumza huku akilia, alisema
kijiji cha Laitimi kipo toka mwaka 1985 bali ni hujuma ya wakubwa wenye
hela ambao wanataka kuhodhi eneo hilo bila kujali utu na haki.
Kwa upande wake, Imamu wa Msikiti wa Laitimi, Hamisi Haji, alilaani bomoabomoa hiyo ambayo haikujali hata nyumba za ibada.Habari na Happiness Mtweve, Dodoma
No comments:
Post a Comment