UPELELEZI
wa kesi inayomkabili Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu
kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, bado haujakamilika.
Hayo
yalielezwa jana na Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao wakati kesi hiyo
ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika au la.Sekwao alidai mahakamani hapo kuwa, upelelezi haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.Baada
ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mmbando aliiahirisha kesi hiyo
hadi Desemba 17, mwaka huu. Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake,
Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu, Sinza Dar es Salaam.Hata
hivyo, umri wake ulizua mvutano mkali baina ya upande wa mashtaka
katika kesi hiyo na jopo la mawakili wanaomtetea, mvutano ambao ulianzia
Mahakama ya Kisutu na kuendelea hadi Mahakama ya Rufani, huku kesi ya
msingi ikiwa haijaanza kusikilizwa.
Juni
11, mwaka huu Mahakama Kuu ilikubali kufanya uchunguzi wa umri halali
wa mshtakiwa, kufuatia maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na jopo
la mawakili wanaomtetea Lulu.
Upande
wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda,
akisaidiana na Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro waliwasilisha maombi
Mahakama ya Rufani wakiomba ifanye marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu,
kama ulikuwa sahihi.
Jopo
la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani lililoongozwa na January Msoffe,
Jaji Bernard Luanda na Edward Rutakangwa, lilizima mvutano na likaamuru
kuendelea kwa kesi ya msingi.
Katika
uamuzi uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma,
jopo hilo kwanza lilisema maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu,
yaliyowasilishwa na Jamhuri yalikuwa batili.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz na picha Irene Mwamfupe Jamii blog.
No comments:
Post a Comment