Hussein Twaha wa Serengeti, akiwatoka wachezaji wa Kongo Brazzaville katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam. Picha kutoka Maktaba ya BIN ZUBEIRY |
NDOTO
za Watanzania kuishuhudia timu yao ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 17, Serengeti Boys inacheza Fainali za Afrika mwakani nchini
Morocco, jana zimeota mbawa baada ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji Kongo
Brazaville mjini Brazaville, Kongo, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao
2-1.
Hata
hivyo, katika mchezo huo wenyeji waliwafanyia vurugu Watanzania tangu
mwanzo wa mchezo ili kuwavuruga kisaikolojia, ingawa hata hivyo vijana
walipigana uwanjani na wanastahili sifa.
Katika
vurugu hizo, Meneja wa Serengeti alipigwa na mashabiki kabla ya mchezo
na hata wakati mchezo ukiendelea Kocha Msaidizi wa Serengeti, Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’ naye alipigwa na Polisi wa Kongo.
Kwa
ujumla mazingira hayakuwa mazuri uwanjani na kutolewa kwa Serengeti leo
hakukuwa kwa kimchezo, bali ubabe wa Wakongo, ambao katika mchezo wa
kwanza walipokewa vizuri na kufanyiwa ukarimu wa hali ya juu mjini Dar
es Salaam wiki mbili zilizopita.
Katika
mchezo wa awali, Serengeti ilishinda 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, bao pekee la beki Mudathir Yahya Abbas kwa shuti la mpira wa
adhabu kutoka umbali wa mita 22 na mpira kabla ya kutinga nyavuni
ulimbabatiza beki mmoja wa Kongo na kumpoteza njia kipa Ombandza Mpea
Joe na kujaa nyavuni.
Faulo
hiyo ilitokana na kiungo wa Serengeti, Hussein Twaha Ibrahim
‘Messi’kuangushwa na beki Okombi Francis wakati akiwa analekea kwenye
eneo la hatari la Wakongo.
chanzo:www.bongostarz.com
No comments:
Post a Comment